Sheria ya Vyombo vya habari yasainiwa Kenya
18 Desemba 2013Matangazo
Sheria hiyo inatoa adhabu kubwa ya faini ya shilingi milioni moja za Kenya kwa mwandishi atakaekutwa na hatia na shilingi milioni 20 kwa chombo kitakachotiwa hatiani. Kutoka mjini Nairobi nimezungumza na Naibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Habari nchini Kenya Victor Bwire ambaye kwanza ana haya ya kusema kuhusu hatua hiyo. Je kusainiwa kwa Sheria mpya ya vyombo vya habari nchini Kenya na rais Uhuru Kenyatta kunaiweka katika nafasi gani sekta ya habari nchini humo?
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman