Sheria kuhusu kima cha chini cha mshara yapasishwa Ujerumani
14 Desemba 2007Matangazo
Bunge la Ujerumani limepasisha sheria ya mshara wa chini kwa wafanyakazi wa Posta.Wanaounga mkono sheria hiyo wanasema sheria ilikuwa inafaa ili kuweza kuhifadhi kazi. Hata hivyo wakosoaji wanatoa hoja kuwa inaweza ikasababisha watu wengi kufutwa kazi.Utoaji wa sheria ya mshahara wa chini kwa wafanyakazi wa Posta wanaotembeza barua katika shirika kuu la Posta hapa Ujerumani la Deutsche Post pamoja na kwa mashirika ya kibnafsi yato ayo huduma za usambazaji mabarua,umekamilisha mvutano wa mda mrefu.Wafanya kazi hao watapata mshahara wa chini wa Euro nane.Sasa kazi nyingine ni kupigania kima cha chini kuwa sawa katika viwanda vyote hapa Ujerumani.