1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sharm el-Sheikh, Misr. Rice atetea uamuzi wa nchi yake.

1 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBdH

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ametetea mapendekezo ya hivi karibuni ya nchi yake ya mauzo na msaada wa kijeshi utakaogharimu mabilioni ya dola kwa ajili ya washirika wa Marekani katika mashariki ya kati kwa kuelezea kuwa mpango huo utasaidia katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Amesema kuwa kuna ajenda muhimu katika upande wa diplomasia na kusisitiza kuwa kuna hatua muhimu pia katika upande wa kidiplomasia, na kwamba hatua hizo zitaambatana na juhudi za kuwasaidia washirika wa Marekani kujilinda dhidi ya kitisho chochote. Kwa hiyo ajenda hii muhimu haimlengi mtu yeyote.

Dr. Rice , ambaye yuko ziarani katika eneo hilo akifuatana na waziri wa ulinzi Robert Gates , alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa kitalii nchini Misr wa Sharm el-Sheikh. Ziara hiyo ya viongozi hao kwa pamoja ni sehemu ya mbinu za kidiplomasia za Marekani kuitenga Iran na kuweza kupata kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa kwa serikali yenye matatizo nchini Iraq inayoungwa mkono na Marekani.

Rice na Gates wamekutana kwa mazungumzo pia katika mji wa pwani nchini saudi Arabia wa Jeddah na mfalme Abdullah wa nchi hiyo.