1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHANGHAI : Rais Köhler amaliza ziara Asia

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxu

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amekamilisha ziara yake nchini China kwa kutowa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano juu ya masuala mbali mbali.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Shanghai cha Tongji Rais Köhler amesema mabadiliko ya hali ya hewa,usambazaji wa nishati na umaskini barani Afrika ni masuala ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka.

Köhler ameyaelezea mazungumzo yake na viongozi wa China ambayo ameyakamilisha mjini Beijing hapo Ijumaa kuwa mazuri sana.

Ziara hiyo ya Rais huyo wa Ujerumani pia imemfikisha nchini Vietnam.