Shambulizi limeua watu 13 Afghanistan
5 Desemba 2007Matangazo
Watu 13 wameuawa katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul baada ya mshambulizi aliejitolea maisha muhanga kulibamiza gari lake lililojazwa miripuko dhidi ya basi lililokuwa limepakia wanajeshi. Miongoni mwa watu hao 13 waliouawa,7 ni raia wa kawaida.
Hilo ni shambulizi la pili la aina hiyo,kufanywa katika kipindi cha siku mbili,tangu Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates kuwasili nchini Afghanistan kwa majadiliano pamoja na Rais Hamid Karzai.Wanamgambo wa Taliban wamejitambulisha kuhusika na shambulizi hilo.