Limetokea katika kituo cha ukaguzi
17 Januari 2017Matangazo
Shambulizi lililofanywa katika kituo cha ukaguzi kusini magharibi mwa Misri limewaua kiasi ya polisi wanane na kuwajeruhi wengine watatu. Vyombo vya serikali ya Misri vimesema shambulizi hilo la risasi limefanyika katika jimbo la el-Wadi el-Gedid kilomita 600 kusini magharibi mwa Cairo. Televisheni ya serikali nchini humo imeripoti kuwa shambulizi hilo lilifanyika jana saa mbili na robo usiku katika kizuizi cha Naqb. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo ingawa kundi la itikadi kalila Dola la Kiisilamu IS limekuwa likidai kuhusika na mashambulizi ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa katika gari , Januari 9, lililofanyika katika kituo cha ukaguzi cha polisi ambapo watu wanane waliuawa.