1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHAM EL SHEIKH: Irak yataka ifutiwe madeni yake

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC56

Waziri mkuu wa Irak Nouri al Maliki ameitolea mwito jamii ya kimataifa iifutie nchi yake madeni ya kigeni.

Bwana Al Maliki ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wenye lengo la kutafuta usalama na kuboresha uchumi wa Irak unaoendelea katika kitongoji cha pwani ya Sham El Sheikh nchini Misri.

Hadi sasa Misri na nchi zingine tatu za ulaya mashariki ndio zimekubali kuifutia Irak madeni yake.

Wakati huo huo bibi Rice ameanza mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Syria Walid al Moualem.

Taarifa zaidi zinafahamisha kwamba mazungumzo hayo yatakwepa maswala nyeti kama vile swala la Lebanon na badala yake yataangazia zaidi maswala ya usalama kati ya Syria na Irak.