Shaka kwa usalama wa vyakula Arusha
9 Novemba 2012Mbunge huyo wa chama cha kijani nchini Ujerumani Ute Koczy ametahadharisha kwamba matumizi ya vumbi la madini ya Uranium kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya kilimo yanaweza kusababisha hatari kubwa kwa wakulima.
Kutokana na hatari kubwa iliyopo mbunge huyo amesema pana haja kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua, angalau kwa ,kutoa habari kwa ukamilifu, "Sisi tunaona pana umuhimu mkubwa kwa serikali ya Tanzania na taasisi mbalimbali kulishughulikia suala hilo.Serikali na taasisi zinapaswa kutoa habari kwa ukamilifu ili watu wajue ni nini kinaweza kutumika na nini kinapaswa kuachwa."
Kwa muda wa miaka mingi mbunge huyo wa Ujerumani Ute Koczy ambae ni msemaji wa wabunge wa chama cha kijani juu ya masuala ya maendeleo amekuwa anafuatilia kwa undani shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium nchini Tanzania. Na hivi karibuni alikuwaa nchini Tanzania ambako aliweza kuijionea mwenyewe shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium . Kutokana na hatari ya vumbi la madini hayo linalotumiwa na baadhi ya wakulima nchini Tanzania, mbunge huyo ameandika barua kwa Shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, na pia kwa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania. Jee ni nini hasa anata katika barua alizoandika? "Nionavyo mimi pana mambo ya kichini chini yanayotokea. Tunaingiwa wasiwasi tunaposikia kwamba wakulima nchini Tanzania wanaanza kutumia vumbi la madini ya uranium ili kuhifadhia mazao yao.Sasa tunaanza kujiuliza jee kinatokea nini nchini Tanzania? alisema mbunge huyo.
Mbunge huyo wa Ujerumani bibi Ute Koczy aliongeza kusema ni hatari kubwa kwa wakulima na kwa watu wengine nchini Tanzania kukaribiana na vumbi la madini ya uranium.
Aidha alisema mpaka sasa hakuna data na takwimu zinazofahamika juu ya viwango vya miali inayoweza kuwa hatari.Kuna habari zinazopingana juu ya hayo. Kutokana hali iliyopo mbunge huyo anataka kupigwa marufuku kabisa kwa matumizi ya vumbi la uranium nchini Tanzania.
Hata hivyo ni vigumu kwa mbunge huyo kusema ni kiasi gani cha vumbi la uranium kinachohusika kwa jumla. Lakini amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yameteoa tahadhari na shirika la nishati ya kiatomiki la Tanzania pia limethibitisha habari hizo.
Mwandishi:Mtullya abdu/Mahojiano Schmidt Andrea.
Tafsiri:Mtullya abdu.
Mhariri:Abdul-Rahman