SEVILLA:mawaziri wa ulinzi wa jumuiya ya NATO wajadili Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEVILLA:mawaziri wa ulinzi wa jumuiya ya NATO wajadili Afghanistan

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za NATOwanakutana leo mjini Sevilla nchini Uhispania kujadili jukumu la majeshi yao nchini Afghanistan.

Kitovu cha majadiliano hayo ya siku mbili ni matayarisho ya mkakati wa kukabiliana na wapiganaji wa kitalibani.

Wadadisi wa masuala ya kijeshi wanaamini kuwa NATO inahijataji askari zaidi ili kuweza kutekeleza jukumu la kulinda amani nchini Afghanistan.

Mkutano huo ni wa kwanza ambapo waziri wa ulinzi wa Marekani bwana Robert Gates atashiriki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com