1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ujerumani yadaiwa kukiuka katiba

Zainab Aziz
15 Novemba 2023

Mahakama ya juu Ujerumani imesema hatua ya serikali ya kubadilisha matumizi ya fedha katika bajeti inakiuka katiba. Juu ya uamuzi huo wa mahakama hiyo

https://p.dw.com/p/4YqGi
Kansela Olaf Scholz wa chama cha SPD
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Mahakama hiyo ya juu iliyoko katika mji wa Karlsruhe imetoa uamuzi huo  kwa kueleza kwamba serikali ya Ujerumani haiwezi kutumia fedha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ambazo zilitengwa kwa ajili ya kupambana na janga la corona.

Mahakama hiyo ya juu imesema ni kinyume cha katiba kupitisha mabadiliko katika bajeti ya nyongeza ya mwaka 2021.

Ujerumani yatangaza mabadiliko ya sheria ya mazingira

Jaji wa mahakama hiyo Doris König wakati wa kutoa hukumu hiyo amesema ni swala la kuzingatia ukomo wa kukopa. Uamuzi huo umewapa ushindi kambi ya Upinzani ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU ambavyo vilipinga hatua ya serikali ya kubadilisha matumizi ya fedha yaliyopitishwa kwenye bajeti.

Kutokana na janga la UVIKO-19 mnamo ya mwaka 2021 serikali ya Ujerumani iliongeza bajeti ya dharura kwa Euro bilioni 60 kwa njia ya mikopo. Katika hali za dharura kama hizo serikali inaweza kuvuka kiwango kinachoruhusiwa kukopa.

Serikali ya muungano ilitaka kuzielekeza fedha katika maswala ya mazingira.

vyama vitatu vya muungano SPD, Kijani na FDP wakiwa Berlin
Viongozi wa serikali ya mseto nchini UjerumaniPicha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Kutokana na kwamba serikali haikuhitaji kiwango hicho cha fedha kukabiliana na janga la corona hata hivyo serikali hiyo ya mseto ya vyama vya SPD, Kijani na chama cha Waliberali FDP, ilitaka kuzielekeza fedha hizo katika maswala ya mazingira. Na baada ya kuidhinishwa na bunge serikali ingeweza kuzielekeza fedha hizo ilikotaka mnamo mwaka 2022.

Maoni: Mwaka mmoja wa Scholz uongozini, sifa zapiku ukosoaji

Wabunge 197 wa kambi ya upinzani waliwasilisha mashtaka hayo kwenye mahakama ya juu mjini Karlsruhe kwa sababu, kwa maoni yao serikali kuu ilijaribu kukwepa ukomo wa kukopa.

Baada ya uamuzi huo wa mahakama ya juu, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema uamuzi huo unaweza kuwa na athari katika mipango ya bajeti. Scholz amelieleza Bunge kwamba serikali sasa inapaswa kutafuta njia nyingine za kupata fedha kwa ajili ya uwekezaji.

dpa/rtre