Serikali ya Merkel yapata pigo kubwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.03.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Serikali ya Merkel yapata pigo kubwa

Matokeo ya chaguzi zilizofanywa jana katika majimbo ya Baden-Württemberg na Rheinland-Pfalz, ni pigo kwa serikali kuu ya Ujerumani mjini Berlin.Serikali hiyo haitoweza tena kuendelea na utaratibu wake kama kawaida.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) nimmt am Montag (28.03.11) in Berlin bei der Sitzung des CDU-Vorstands Platz. Der Vorstand der CDU kam am Montag nach den Landtagswahlen vom Sonntag (28.03.11) in Baden-Wuerttemberg und Rheinland-Pfalz zu einer Sitzung zusammen. (zu dapd-Text). Foto: Berthold Stadler/dapd

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa chama cha CDU

Licha ya matokeo ya chaguzi hizo mbili kuwa pigo kubwa kwa serikali ya muungano, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa chama cha kihafidhina cha CDU, anaweza kuwa na matumaini ya kujitoa katika janga la chaguzi hizo. Ataweza kurejesha imani ya umma ikiwa atafanikiwa kuibadili sera ya serikali yake kuhusu nishati ya nyuklia na badala yake kuzingatia nishati mbadala. Sasa anapaswa kuchukua hatua za dhati kuweka misingi itakayosaidia kuimarisha uzalishaji wa nishati mbadala katika majimbo yanayotawalwa na vyama vya serikali kuu. Kwa mfano, kujenga mabwawa ya vinu vya nishati, kuruhusu miundo mbinu mipya ya kusambaza nishati mbadala na kadhalika.

Kama kiongozi wa chama cha kisoshalisti cha SPD alivyotambua, wapiga kura katika chaguzi za hiyo jana, walionyesha wazi wazi kuwa wanapinga nishati ya nyuklia. Mwanasiasa ye yote yule serikalini aliekuwa na matumaini kuwa hali itaendelea kama kawaida baada ya kutangaza kuifanyia uchunguzi baadhi ya mitambo ya nishati ya nyuklia na kuifunga ikihitajika, basi huyo amekosea.

Free Democratric Party (FDP) Chairman and German Foreign Minister Guido Westerwelle addresses the media in Berlin on Monday, March 28, 2011. The Free Democrat's had lost about the half of their votes in the regional state elections in Baden-Wuerttemberg and Rhineland-Palatinate on Sunday. (AP Photo/Markus Schreiber)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle alie mwenyekiti wa FDP

Ni dhahiri kuwa vyama vinavyotawala katika serikali kuu havitokubali kiholela mageuzi katika sera za nishati. Kansela Merkel hana budi kujiandaa kwa midahalo mikali ndani ya vyama hivyo. Lakini Merkel hadi sasa, amefanikiwa kuwashawishi wanachama wenzake wa CDU hata katika masuala yanayohusika na mageuzi makubwa, kama vile kuondoshwa utaratibu wa vijana kulitumikia jeshi muda maalum. Kwani yule anaeweza kusimama kidete na kwenda kinyume na mkuu wa chama, bado hajaonekana katika chama hicho cha CDU.

Hali ya mambo ni hiyo hiyo hata katika chama cha kiliberali cha FDP, jambo ambalo kwa sasa ndio linalomnusuru mkuu wa chama hicho, Guido Westerwelle. Wachache walio na uwezo wa kumrithi, kama vile katibu mkuu wa chama, Lindner, au waziri wa afya, Rösler, kwa sasa wanachukuliwa kuwa bado ni vijana mno na hawana ujuzi wa kutosha kushika usukani wa chama kilichozongwa na mizozo. Kwa hivyo, hivi sasa serikali ya Merkel na Westerwelle itaendelea kufanya kazi, lakini kwa masharti magumu.

 • Tarehe 28.03.2011
 • Mwandishi Stützle,Peter/ZPR/P.Martin
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RDQZ
 • Tarehe 28.03.2011
 • Mwandishi Stützle,Peter/ZPR/P.Martin
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RDQZ

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com