Serikali mpya Ugiriki
9 Novemba 2011Serikali mpya ya mpito Ugiriki itatangazwa hii leo.Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo.
Mazungumzo yalioingia siku ya tatu ya kuunda serikali hiyo mpya yalisita hapo jana jioni, pasi kutajwa waziri mkuu mpya atakaye mrithi yule anayeondoka, Gerge Papandreou. Papandreou na kiongozi wa upinzani Antonis Samaras, walifanya mazungumzo siku nzima ya Jumatatu.
Aliyekuwa makamu wa rais wa benki kuu ya Ulaya, Lucas Papademos, huenda ndiye atakayekuwa waziri mkuu mpya. Papandreou amekubali kujiuzulu punde tu makubaliano yatakapofikiwa.
Serikali ya mpito itakuwa na jukumu la kutekeleza mageuzi yalioitishwa na Umoja wa Ulaya na shirika la kimataifa la fedha, IMF, ili nchi hiyo inayokumbwa na madeni iweze kupokea mkopo.
Mwandishi Maryam Abdalla/all