Serbia yawafungulia mashitaka viongozi wa Kosovo
18 Februari 2008Matangazo
Wizara ya mambo ya ndani ya Serbia imewasilisha mashitaka ya uhalifu dhidi ya viongozi wa Kosovo kwa kutangaza uhuru wa nchi ambayo haipo katika ardhi ya Serbia. Miongoni mwa walioshtakiwa ni rais wa Kosovo Fatmir Sejdiu na waziri mkuu Hashim Thaci.
Serikali ya Belgrade inasema itazuia juhudi za Umoja wa Mataifa na muungano wa usalama na ushirikiano barani Ulaya kuitambua Kosovo.