1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia haitotumia nguvu kuhusu Kosovo

15 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D7nz

NEW YORK:

Serbia haitotumia nguvu iwapo jimbo lake la kusini Kosovo litajitangazia uhuru wake.Waziri wa Nje wa Serbia Vuk Jeremic alitamka hayo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York.Amesema,nchi yake lakini itatumia njia zote zilizopo ikiwa ni za kiuchumi,kisiasa na kibalozi,ili kuzuia jimbo hilo la kusini kujitoa kutoka Serbia.Urusi inayopinga pia uhuru wa Kosovo iliitisha kikao maalum cha Baraza la Usalama kujadili suala hilo.Inaaminiwa kuwa Kosovo itajitangazia uhuru wake siku ya Jumapili au Jumatatu ijayo.Marekani na baadhi kubwa ya nchi wanachama katika Umoja wa Ulaya,Ujerumani ikiwa mojawapo,zipo tayari kulitambua taifa jipya.Umoja wa Ulaya unatayarisha ujumbe maalum kwa azma ya kulisaidia jimbo hilo kuelekea uhuru wake.Ujumbe huo utakuwa na kama watu 2,000 wengi wao wakiwa polisi na wataalamu wa sheria.