1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera ya pamoja ya Ulinzi barani Ulaya, Pesco, magazetini

Oumilkheir Hamidou
14 Novemba 2017

Mpango wa Umoja wa Ulaya wa kubuni mkakati wa pamoja wa ulinzi, jinsi mashambulio ya kigaidi yanavyoathiri uzoefu wa maisha ya wafaransa na mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/2nakS
Belgien Treffen der EU Außen- und Verteidigungsminister
Picha: Reuters/E. Dunand

Tunaanzia Brussels ambako matumaini makubwa yamechomoza kuona siku moja Umoja wa sarafu ukifuatiwa na Umoja wa ulinzi. Gazeti la "Badische Zeitung" linaandika: "Sera ya pamoja ya ulinzi iliyopewa jina PESCO inazusha matumaini makubwa. Sio tu kwa sababu, kwa namna hiyo gharama zitapungua na kujitegemea zaidi mbele ya sera ya nje ya Donald Trump au atakayeshika nafasi yake mjini Washington, bali pia kwa sababu itazipatia nchi za Umoja wa ulaya mada inayoziunganisha na ambayo wanaihitaji kupita kiasi. Majukumu mengine makubwa, na hasa sera za uhamiaji, yanazusha mivutano badala ya kusaidia kuimarisha mshikamano kati ya mashariki na magharibi, na kaskazini na kusini."

Pesco usiishie kabatini

Gazeti la mjini Bremen "Weser-Kurier" linaonya mpango huo usije ukamalizikia kabatini. Gazeti linaendelea kuandika: "Kama hatimaye utaundwa kweli umoja wa ulinzi barani Ulaya, hilo sio suala hasa watu wanalojiuliza. Zaidi kuliko yote, wanajiuliza kama mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya yatahakikisha, mpango huo unaobidi kutiwa saini mawaziri wa ulinzi  wa Umoja wa ulaya watakapokutana hivi karibuni, haubakii gamba tu.

Jinsi mashambulio ya kigaidi yanavyoathiri maisha ya wafaransa

Ufaransa ina sifa ya kuwa nchi inayotanguliza mbele, uhuru, udugu na usawa. Maadili hayo yamebadilika kutokana na mashambulio ya kigaidi, linahisi gazeti la "Aachener Nachrichten linaloandika."Usalama badala ya uhuru: Maadili ya Ufaransa yamewekwa kando kutokana na vitisho vilivyoko. Badala yake wanatanguliza mbele usalama badala ya uhuru. Wafaransa wanalazimika kujidhili katika masuala ya haki za binaadam, jambo ambalo miaka ya nyuma kamwe lisingewezekana. Na hali hiyo haitarajiwi kubadilika haraka hivyo kutokana na vitisho vinavyoselelea.

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi waingia awamu muhimu

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaendelea mjini Bonn. Wahariri wanahisi hakuna makubwa ya kutegemea. Gazeti la "Darmstädter Echo" linazungumzia moshi wa sumu unaotoka viwandani na kuandika:"Baada ya wachunguzi kuchapisha ripoti yao inayofafanua hali namna ilivyo, hakuna tena kudanganyana. Na hali hiyo inauhusu mkutano wa mabadiliko ya tabianchi  unaoingia katika awamu muhimu kesho jumatano. Sawa na inavyoyahusu mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano wa vyama vinne mjini Berlin ambako wawakilishi wa vyama vya CDU, CSU, FDP na die Grüne wanabishana kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Kutegemea kwamba kiu cha nishati cha jamhuri ya umma wa China kitapungua, haitoshi na hilo kila mmoja anabidi alitambue. Na ni ujinga pia kutegemea kwamba jamhuri ya umma wa China, itageuka mshika bendera wa wanaopigania usafi wa mazingira, baada ya Marekani kujitenga.

 

Mwanndishi:Hamidou Oumilkheir/Inlanadspresse

Mhariri:Josephat Charo