Seoul.Hali ya mawasiliano inarejea taratibu. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Seoul.Hali ya mawasiliano inarejea taratibu.

Mawasiliano ya simu katika eneo la Asia taratibu yanarejea katika hali ya kawaida baada ya tetemeko la ardhi katika pwani ya Taiwan kuharibu waya na kusababisha watu kadha kutokuwa na mawasiliano ya internet.

Simu nyingi katika eneo la Asia pamoja na internet zimerejea katika hali ya kawaida lakini hali katika baadhi ya sehemu za Korea ya kusini na Taiwan bado si nzuri.

Mashirika makubwa ya simu na internet katika eneo hilo yameonya kuwa kazi ya ukarabati itachukua zaidi ya wiki.

Tetemeko hilo lililokuwa katika kipimo cha 7.1 katika kipimo cha richter liliikumba eneo la pwani ya kusini ya Taiwan siku ya Jumanne, na kuuwa watu wawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com