SEOUL: Wito kuachilia huru mahabusu wa Korea ya Kusini | Habari za Ulimwengu | DW | 21.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEOUL: Wito kuachilia huru mahabusu wa Korea ya Kusini

Rais wa Korea ya Kusini,Roh Moo Hyun ametoa wito wa kuwaachilia huru moja kwa moja wananchi wenzake 23,waliotekwa nyara siku ya Alkhamisi, nchini Afghanistan.Amesema,kwa hali yo yote ile kusitokee hasara ya maisha.Alipozungumza kwenye televisheni kulihotubia taifa,Rais Roh alisema, serikali yake ipo tayari kujadiliana na wahusika, ili raia wa Korea ya Kusini wapate kuachiliwa huru,upesi iwezekanavyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com