1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL : Treni zavuka mpaka wa Korea

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1C

Treni mbili zimevuka kanda yenye ulinzi mkali wa kijeshi ambayo inazitenganisha Korea ya Kaskazini na ya Kusini kwa mara ya kwanza kabisa tokea vilipoanza vita vya Korea hapo mwaka 1950.

Treni iliotokea Korea ya Kusini ilisindikizwa kwa fataki na mamia ya watu waliokuwa wakipeperusha bendera.Majaribio ya safari hizo za reli kwenye njia mbili za reli zilizokarabatiwa upya katika maeneo ya magharibi na mashariki ya bara la Korea yanakuja baada ya kucheleweshwa mara kadhaa tokea njia hizo za reli zilipounganishwa miaka minne iliopita.

Korea Kusini imetowa msaada wa kama dola milioni 80 kwa viwanda vidogo vidogo vya Korea Kaskazini kuishawishi serikali ya nchi hiyo kuruhusu safari hizo za reli.