SEOUL : Korea Kaskazini yaanza kuufunga mtambo | Habari za Ulimwengu | DW | 17.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEOUL : Korea Kaskazini yaanza kuufunga mtambo

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema yumkini ikawa imeanza kuufunga mtambo wake wa nuklea.

Repoti zinasema picha za upelelezi za sataliati za Marekani zimeonyesha kuongezeka kwa harakati kwenye mtambo wa nuklea wa Yongbyon nchini Korea Kaskazini.Maafisa wa serikali ya Korea Kusini wamekataa kuzungumzia repoti hiyo.Serikali ya Korea Kusini imekuwa ikifikiria kusitisha utowaji wa msaada zaidi wa mchele kwa Korea Kaskazini hadi hapo nchi hiyo itakapoanza mchakato wa kuufunga mtambo wake huo wa nuklea.

Kufungwa kwa mtambo huo kumekuja siku kadhaa baada ya kupita kwa muda wake kama ilivyokuwa imetakiwa chini ya makubaliano ya mataifa sita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com