1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneti la Marekani kupiga kura kuhusu mpango mpya wa uchumi

Kalyango Siraj1 Oktoba 2008

Je Utapita leo?

https://p.dw.com/p/FSBC
Maseneta wa baraza la Senate la Marekani Chris Dodd, kushoto, na Judd Gregg, kulia.Kuna matumaini kuwa baraza hilo litapashisha muswada mpyaPicha: AP

Baraza la Senate la Marekani litapiga kura baadae leo kuhusu mpango wa serikali wa dola billioni 700 uliofanyiwa marekebisho wa kuupiga jeki mfumo wa fedha wa Marekani.

Mpango wa mwanzo ulikataliwa na baraza la wawakilishi mapema wiki hii.

Maelezo zaidi kuhusu mpango huo mpya baado ni finyu kwa kuwa ulikuwa baado unapikwa mjini Washington kufikia jana jioni kufuatia kutangazwa katika bazala la seneti.

Hatua ya leo jumatano inafuatia hatua ya baraza la wawakilishi kuukata muswada huo jumatatu kwa kura 228 zinazopinga ilhali kura 205 kuunga mkono. Inasemekana kuwa wengi wa walioukataa ni wabunge wa Republican.

Lakini inatarajiwa kuwa muswaada huu ambao umefanyiwa marekebisho utapasishwa kama alivyogusia mmoja wa wajumbe wa Republican Seneta Judd Gregg.Alisema kuwa anadhani baraza la Seneti litaupasisha kwani kuna makubaliano kuwa kuna mgogoro unaotaka hatua za dharura.

Matokeo ya kura ya jumatatu yalipelekea mporomoko mbaya kuwahi kutokea katika soko la hisa la Marekani kwa kipindi cha miaka 21.

Na kutokana na hayo huenda ndio inapelekea baadhi ya wabunge wa baraza la wawakilishi ambao walikuwa wanaupinga kubadili nia yao na badala yake kutoa mwito wa kuupasisha.Mmoja wao ni mbunge wa chama cha democrat-Bobby Scott. Amesema kuwa ni lazima wapasiashe kitu.

Ikiwa baraza la seneti litapasisha muswaada huo uliofanyiwa marekebisho,kama inavyotarajiwa ,hali hiyo itazidisha mbinyo kwa baraza la wawakilishi nalo kuweza kuupasisha litakapokutana tena kesho alhamisi.

Mpango huo unaungwa mkono na rais Bush,waziri wake wa fedha,Henry Paulson pamoja na wagombea wawili wa kiti cha uraisi nchini Marekani,John McCain na Barack Obama.

Miongoni mwa mabadiliko yaliyooongezwa katika muswada huu mpya ambao utapigiwa kura na baraza la seneti leo jumatano ni kifungu cha nyongeza ya dhamana ya serikali kwa amana za benki kutoka dola laki moja hadi dola laki moja na nusu.

Huenda hilo ndilo mojawapo wa sababu zilizopelekea wanasiasa kama vile Obama kusema mpango huo ni sawa.

Kutokana na taarifa kuwa muswada huo utapigiwa kura leo jumatano katika baraza la seneti na uwezekano wa kura ya ndio kutokea,sasa masoko ya hisa ya Marekani yamepanda bei ambapo faharasa 500 za Standard & Poor zilipanda zaidi ya 5%,kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea kwa siku moja katika kipindi cha miaka sita ya kampuni hiyo.