1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal na Mali magazetini

1 Aprili 2012

Matokeo ya uchaguzi nchini Senegal,mapinduzi ya kijeshi nchini Mali,na juhudi za kupambana na maharamia wakisomali ni miongoni mwa mada katika magazeti ya ujerumani kuhusu bara la Afrika wiki hii.

https://p.dw.com/p/14W1j
Wasenegal washangiria ushindi wa mgom,bea wao Macky SallPicha: REUTERS

Tuanzie Senegal ambako,sawa na Mali ,magazeti takriban yote mashuhuri yamechambua matokeo ya uchaguzi wa rais wiki hii.Hatamu za uongozi zabadilishwa kwa amani nchini Senegal,Sall amuwekea mtego "mzee" ni miongozi mwa vichwa vya habari magazetini kuhusu Senegal.Lilikuwa gazeti la mjini Berlin,Die Tageszeitung lililoandika kuhusu kile mhariri wa gazeti hilo alichokiita "Mtego wa Sall kwa mzee",akizungumzia jinsi rais Abdoulaye Wade mwenye umri wa miaka 85 alivyoungama kwamba ameshindwa baada ya miezi kadhaa ya machafuko barabarani na pigo katika vituo vya uchaguzi.

Senegal inajipatia rais mpya,Macky Sall-kiongozi wa upande wa upinzani aliyemshinda mtetezi wa wadhifa huo wa rais Abdoulaye Wade.Hata kabla ya matokeo yote kutangazwa mzee Wade alimpigia simu Sall mwenye umri wa miaka 50 na kumpongeza.Ushindi huo umewezekana baada ya vyama takriban vyote vya upinzani kujiunga na Macky Sall kwa kile wenyewe wanachokiita" Bennoo Bokk Yaakar"-au "muungano kwaajili ya mageuzi."

Gazeti la Berliner Zeitung limezungumzia pia kuhusu mageuzi ya uongozi kwa njia ya amani nchini Senegal .Rais mpya Macky Sall ameahidi kupunguza bei za vyakula linasema gazeti hilo linalolinganisha pongezi za rais aliyeshindwa Abdoulaye Wade kwa waziri mkuu wake wa zamani Macky Sall na zile alizopewa yeye mwenyewe miaka 12 iliyopita na mtangulizi wake Abdou Diouf,baada ya kukalia viti vya upande wa upinzani kwa zaidi ya miaka 20 hapo awali.

Flüchtlinge aus Mali in Flüchtlingslager in Niger
Wakimbnizi wa Mali nchini NigerPicha: Fatoumata Diabate

Mbinu za Wade kutaka kugombea kwa mara ya tatu wadhifa wa rais,kinyume na katiba,zilitishia kuzusha mzozo mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo inayosifiwa kama mfano wa kuigizwa wa demokrasia barani Afrika.Watu wasiopungua sita wameuwawa kufuatia maandamano dhidi ya uamuzi wa Wade wa kugombea kwa mara ya tatu kiti cha rais.

Nafasi za kazi zinahitajika na hasa kwa vijana walioandamana dhidi ya Wade linamalizika kuandika gazeti la Berliner Zeitung linalozungumzia jinsi jumuia ya kimataifa ilivyosifu jinsi duru ya pili ya uchaguzi ilivyopita.

Mada ya pili iliyohanikiza magazetini nchini Ujerumani wiki hii inahusu mapinduzi ya kijeshi katika nchi nyengine iliyokuwa na sifa za kukomaa kidemokrasi barani Afrika-Mali.

Lilikuwa gazeti la Die Zeit lililojiuliza kama kifo cha Gaddafi kina uhusiano wowote na mapinduzi nchini Mali.Kwa mujibu wa Die Zeit linalonukuu maelezo yaliyoenea katika mji mkuu wa Mali-Bamako- Amadou Sanogo anaeongoza mapinduzi hayo,hakuwa amedharimia kuingia katika kasri la rais na kuitia dowa demokrasia iliyokuwa ikisifiwa sana na nchi za magharibi ya Mali.Kuhusu hatima ya Sanogo na kamati yake iliyoundwa kwa pupa ya kurejesha demokrasi na nidhamu,hakuna anaeweza kuashiria.Kuhusu mtu mwengine ambae huenda amekamata nafasi muhimu,kuna la kusema,kwakuwa au pengine kwasababu ameshafariki tangu miezi sita iliyopita-Muammar Gaddafi.

Gazeti la Die Zeit linasema Kwa miongo kadhaa Mali ilikuwa ikijulikkana kama eneo la ushawishi mkubwa la yule aliyejipa jina la Mfalme wa Afrika.

Baada ya Gaadfi kuanguka, mamluki wa kituareg wamerejea katika nchi za kanda ya Sahel,wakibeba silaha za kimambo leo kutoka Libya.Kaskazini mwa Mali waasi hao wa kituareg wanapigana dhidi ya vikosi vilivyozidiwa vya serikali.Hiyo ndio sababu ya malalamiko ya Sanogo na wanajeshi wake,linaandika Die Zeit.Hawakutaka kuhusishwa na mzozo ambao tokea hapo wasingeweza kushinda na ambao wakihisi rais Toumani Toure angeweza kuufumbua kwa njia ya mazungumzo.Ndio maana hatua ya kwanza ya Sanogo,linaandika Die Zeit ilikuwa kupendekeza mazungumzo ya amani pamoja na waasi.Hata hivyo linamaliza kuandika Die Zeit kurejea nyumbani mamluki walikuwa Libya sio chanzo cha mzozo wa Mali,bali wameupalilia tu.

EU NAVFOR Mission Piraten
Tume ya Umoja wa Ulaya ya kupambana na maharamia wa kisomaliPicha: www.eunavfor.eu

Frankfurter Allgemeine Zeitung linazungumzia kishindo kinachowakabili wanajeshi warejee kambini.Nalo Die Tageszeitung linasema viongozi wa mataifa ya jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi Afrika Magharibi ECOWAS wameshaonya wanajeshi wao wanaweza ikilazimika kuingilia kati nchini Mali.

Lilikuwa gazeti la Financial Times Deuschland lililozungumzia kuhusu juhudi za kupambana na maharamia katika fukwe za Somalia.Gazeti linasema mapambano ya habarini hayatoshi.Gazeti linahisi mapambano dhidi ya maharamia yanaweza kufanikiwa ikiwa walioko nyuma ya maharamia watashindwa nguvu.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/DW-Pressedatenbank

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman