1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEBHA : Gaddafi adhihaki demokrasia ya magharibi

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN4

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi hapo jana ameidhihaki dhana ya demokrasia ya mataifa ya magharibi katika hotuba ya kuadhimisha miaka 30 ya kuanzishwa kwa Libya Jamahiriya Taifa la Umma.

Kiongozi huyo wa Kiarabu alietawala kwa muda mrefu amesema chaguzi ni upuuzi kwamba sio upigaji kura wenye kuhakikisha kuwepo kwa demokrasia.Amesema mfumo wa uchaguzi katika mataifa ya magharibi unaweza kushajiisha udanganyifu na ununuwaji wa kura kwa hiyo hauko wazi.

Akihutubia kikao maalum cha bunge huko Sebha kilomita 1000 kusini mwa mji mkuu wa Tripoli kilichohudhuriwa na marais wa Chad,Uganda na Niger Gaddafi pia ameushutumu mfumo wa fedha duniani kuwa ni udikteta chini ya msingi wa hofu ambapo mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi huyatia hofu mataifa mengine kwa kuyafanya yawe na njaa na kugomea mali zao ghafi kama vile kahawa na mafuta.