SARAJEVO: Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SARAJEVO: Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi

Aliyekuwa waziri wa mamboya kigeni wa Bosni wakati wa vita, Haris Silajdzic, anaongoza mbele ya mpinzani wake, Sulejman Tihic, katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa Bosnia.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema huku asilimia 40 ya kura zikiwa zimehesabiwa, Silajdzic amejipatia asilimia 38 ya kura dhidi ya Tihic aliyepata asilimia 18.

Raia wa Bosnia walijitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi watakaoongoza serikali ya kwanza ya taifa hilo la Balkan wakati usimamizi wa kimatiafa utakapomalizika mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com