SAO PAULO.Mama aliyemwuua mtu aliyembaka mwanawe achiwa huru
15 Novemba 2006Matangazo
Mama mmoja aliemwuuwa mtu aliembaka mtoto wake wa kiume ameachiwa huru nchini Brazil.
Mahakama ya mjini Sao Paulo imepitisha uamuzi huo kwa kueleza kwamba mwanamke huyo bibi Maria do Carmo Ghislotti alimwuua mbakaji huyo ili kutetea haki ya mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu.
Bibi Maria Ghilotti alimwuuwa mhalifu huyo kwa kutumia sime.