SAO PAULO: Maandamano ya kupinga ziara ya Bush yafanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SAO PAULO: Maandamano ya kupinga ziara ya Bush yafanyika

Maelfu ya waandamanaji nchini Brazil wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuwasili kwa rais George W Bush wa Marekani nchini humo. Ingawa maandamano hayo yalikuwa ya amani, mapigano baina ya polisi na waandamanaji hao yamesababisha watu zaidi ya 20 kujeruhiwa.

Baadaye leo rais Bush atakutana na raia wa Brazil, Ignacio Lula da Silva, kusaini mkataba wa matumizi ya mafuta aina ya ethanol.

Nchini Colombia ambako rais Bush anatarajiwa kuwasili keshokutwa Jumapili, wanafunzi, wafuasi wa vyama vya upinzani na na wanachama wa vyama vya wafanyakazi wamekuwa wakifanya maandamano kwa siku mbili kuipinga ziara ya Bush nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com