SAN DIEGO: Rais Bush atembelea eneo la maafa
26 Oktoba 2007Matangazo
Rais wa Marekani,George W.Bush ametembelea jimbo la Kalifornia kujionea mwenyewe hasara iliyosababishwa na mioto.Bush alikuwa pamoja na Gavana wa Kalifornia,Arnold Schwarzenegger.Karibu na mji wa San Diego,zaidi ya nyumba 8,500 zipo hatarini.Hadi hivi sasa si chini ya watu 500,000 wamelazimika kuondoka majumbani mwao.