Sakata ya mafuta Visiwani Zanzibar
29 Aprili 2009Matangazo
Hivyo, kukazuka majadiliano makali kama mafuta hayo pindi yakichimbuliwa yasimamiwe na kumilikiwa na serikali ya Muungano wa Tanzania au na ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini jana Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alisema kwamba hakujagunduliwa mafuta Zanzibar. Ikiwa ni hivyo, jee kulikuweko haja ya mabishano juu ya jambo hilo yaliozagaa hapo kabla huko Zanzibar?
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman
Othman Miraji alimpigia simu waziri wa nishati wa serikali ya Zanzibar, Mansur Yusuf Himid, ili kupata ufafanuzi zaidi...