SACRAMENTO : Steinmeir yuko California
30 Agosti 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir amewasili katika jimbo la Carlifonia nchini Marekani kwa mazungumzo na gavana wa jimbo hilo Arnold Schwarzenegger.
Mkutano wao katika mji mkuu wa jimbo hilo Sacramento unatagemewa kulenga mabadiliko ya hali ya hewa na uwezekano wa kuratibu mabadilishano ya mifumo ya utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira barani Ulaya na Marekani.