1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAARBRÜCKEN : Kesi ya mauaji ya ngono kwa mtoto yamalizika

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRw

Nchini Ujerumani kesi iliodumu kwa miaka mitatu juu ya kutoweka kwa mvulana wa miaka mitano imemalizika kwa kuachiliwa huru kwa watuhumiwa wote.

Hakimu katika mji wa kusini mwa Ujerumani wa Saarbrücken ametowa hukumu ya kuachiliwa kwao kwa kusema kwamba kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwaona watuhumiwa hao 12 wana hatia.Wanaume wanane na wanawake wanne walikuwa wametuhumiwa kwa kumfanyia shambulio la ngono na baadae kumuuwa mvulana huyo Pascal kwenye kilabu cha pombe hapo mwaka 2001.

Mwili wa mvulana huyo haukuweza kupatikana.