Rwanda: Mkutano kuhusu Adhabu ya Kifo
24 Septemba 2009Matangazo
Mojawapo ya mijadala hiyo umeanza mjini Kigali nchini Rwanda, ukiwahusisha wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini.
Kaimu kamishna wa Tume ya AU ya haki za binadamu, Bahami Tom Nyanduga ambaye anauongoza mjadala huo, amesema lengo la umoja wa Afrika ni kufikia itifaki itakayozilazimu nchi wanachama wote kuiondoa adhabu kwenye sheria zake siku za usoni.
Daniel Gakuba amehudhuria mkutano huo na kututumia taarifa ifuatayo.