1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rouhani ataka kupanua uhuru wa watu binafsi Iran

Sekione Kitojo
8 Januari 2018

Maandamano yaliyoitikisa Iran hayalengi tu uchumi,rais Rouhani amesema,akiashiria lengo maalum kuwa dhidi ya wahafidhina wenye nguvu wanaopinga mpango wake wa kupanua uhuru wa watu binafsi na kuhimiza maridhiano ya nje.

https://p.dw.com/p/2qWP7
Deutschland Nürnberg - Exil-Iraner Solidaritätsaktion proteste Iran
Picha: UGC/Siavash Arabkhani

Taarifa  kamili  na  Sekione Kitojo.

Kiongozi  huyo , ambaye  alimshinda mgombea  ambaye  ni mwenye  msimamo  mkali  wa  kupinga mataifa  ya magharibi  na  kushinda  uchaguzi mpya  mwaka , pia alitoa  wito wa   kuondolewa  kwa  vizuwizi  katika mitandao  ya  kijamii  inayotumiwa  na  waandamanaji wanaoipinga  serikali  katika  changamoto  kubwa  ya muda  mrefu  kwa  maafisa  wenye  msimamo  mkali  tangu mwaka  2009.

"ilikuwa  ni  uwasilishaji  usiofaa  wa  matukio  na  pia  tusi kwa  watu  wa  Iran  kusema  walikuwa  tu  na  madai  ya kiuchumi," Rouhani  alinukuliwa  akisema  na  shirika  la habari  la Tasnim.

Iran Müllsucher
Mkaazi wa mji mmoja nchini Iran akitafuta vitu katika mapipaPicha: ilna

"watu  walikuwa  na  madai ya  kiuchumi, kisiasa  na kijamii."

Jeshi  la  Iran  lenye  ushawishi  mkubwa  la   mapinduzi , lilisema  jana  Jumapili  kuwa  majeshi  ya  usalama yamefikisha  mwisho  machafuko  ya  wiki  nzima yaliyochochewa  na  kile  ilichosema  maadui  ya  nje.

Maandamano, ambayo  yalianza  kuhusiana  na  ugumu wa  maisha yanayowakumba  vijana  na   tabaka  la wafanyakazi, yalisambaa  hadi  katika  zaidi  ya  miji  80  na yalisababisha  vifo  vya  watu  22  na  zaidi  ya  wengine 1,000  walikamatwa, kwa  mujibu  wa  maafisa  nchini  Iran. Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa  Iran Javad Zarif amesema ni  wazo lisilokubalika  kwa  nchi  jirani  kuidhoofisha  nchi yake.

Mohammad Javad Zarif Außenminister Iran
Mohammad Javad Zarif waziri wa mambo ya kigeni wa IranPicha: picture-alliance/dpa/A. Novoderezhkin

Hakuna  nchi  inaweza  kujipatia  usalama  pekee yake kwa kuidhoofisha  nchi  jirani. Ni  wazo  la  hatari  katika duniani  hii ya  utandawazi.

Viongozi wa mandamano wametambuliwa

Hamid Shahriari , naibu mkuu  wa  mahakama  alisema kwamba  viongozi  wote  wa  maandamano  wametambulika na  kukamatwa, na  wataadhibiwa  vikali na  huenda wakakabiliwa  na  adhabu  ya  kifo.

Mbunge mmoja wa Iran  amethibitisha leo kifo  cha  mmoja kati  ya  wafungwa  waliokamatwa.

"Kijana  huyo  wa  miaka  22  alikamatwa  na  polisi. Nilifahamishwa  kwamba  alijiua akiwa  jela, " Tayebeh Siavashi  alinukuliwa  akisema  na  shirika  la  habari  la ILNA.

Waandamanaji  wengi  walihoji  sera  za  mambo  ya  kigeni za  Iran  katika  mashariki  ya  kati , ambako  nchi  hiyo inaingilia  nchini  Syria na  Iraq  katika  vita  kwa  ajili  ya kujipatia  ushawishi  dhidi  ya  hasimu  wake  Saudi  Arabia.

Msaada  wa  kifedha  kwa  Wapalestina  na  kundi  la Washia  la  Lebanon  pia  umewakasirisha  Wairani, ambao wanataka  serikali  yao  kuaangalia  zaidi  kuhusu  matatizo ya  ndani  badala  ya  kusaidia  mataifa  ya  nje.

Akirejea  baadhi  ya  matamshi  yake  katika  kampeni, Rouhani  alisema  leo  kwamba  watu wanapaswa kuruhusiwa  kuwakosoa  maafisa  wote  wa  Iran , bila kubagua.

Iran Rohani 100-Tage-Bilanz der Regierung
Rais wa Iran Hassan RouhaniPicha: irna.ir

Awali waandamanaji  walielekeza  hasira  yao  kuhusiana na  bei  ya  juu  ya  bidhaa  pamoja  na  madi  ya  kuwapo na  rushwa , lakini  maandamano  hayo yalichukua mkondo  mwingine   wa  kisiasa , ambapo  idadi  kubwa  ya watu  walimtaka  kiongozi  mkuu  wa  kidini  nchini  humo Ayatollah Ali Khamenei  ajiuzulu.

Kiongozi  huyo  mkuu  ni amiri  jeshi  mkuu  wa  majeshi  ya ulinzi  na  anateua  viongozi  wa  mahakama.Mawaziri muhimu wateuliwa  kwa  makubaliano  nae  na  ana  kauli ya  mwisho  kuhusiana  na  sera  za  mambo  ya  kigeni  ya Iran. Kwa  ulinganisho , rais  ana  madaraka  madogo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman