ROMA:Romano Prodi aponea chuchupu kura ya imani | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROMA:Romano Prodi aponea chuchupu kura ya imani

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi ameshinda kwa wingi mdogo kura ya kuwa na imani naye katika bunge la seneti na hivyo kubakia kama waziri mkuu wa nchi hiyo.Hata hivyo Prodi anakabiliwa na kura nyingine kama hiyo kwenye bunge dogo.Prodi alijiuzulu wiki iliyopita baada ya miezi tisa ya kuingia madarakanikutokana na kushindwa kwenye kura ya bunge la seneti juu ya sera zake za nje.

Serikali ya Prodi iliunga mkono mswaada wa kuongeza wanajeshi wa Italia nchini Afghanstan pamoja na kukubali upanuzi wa kituo cha kijeshi cha Marekani katika eneo la Vicenza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com