1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Waumini waliokwenda kuhiji wamefariki katika ajali ya basi

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCky

Waingereza 2 wamefariki na wengine 25 wamepelekwa hospitali wakiwa na majeraha,kufuatia ajali ya basi lililokuwa likisafirisha watu waliokwenda kuhiji nchini Saudi Arabia.Basi hilo lilipata ajali kama kilomita 90 kaskazini ya mji wa Jeddah lilipokuwa likisafiri kati ya miji takatifu ya Medina na Mekka.Kila mwaka kiasi ya Waingereza 25,000 huenda kuhiji Mekka.