RIYADH: Wanachama wa OPEC wakutana Saudi Arabia
16 Novemba 2007Matangazo
Mkutano wa kilele wa OPEC-shirika la nchi zinazozalisha mafuta ya petroli,utafanywa mjini Riyadh,Saudi Arabia kuanzia Novemba 17 hadi 18. Mawaziri wa mafuta wamesema,mkutano huo wa kilele hautopitisha uamuzi juu ya sera ya muda mfupi, kuhusika na uzalishaji wa mafuta.Mada hiyo, itajadiliwa kwenye mkutano utakaofanywa Desemba 5 mjini Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu.