RIYADH: Musharraf awasili Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH: Musharraf awasili Saudi Arabia

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amewasili mjini Riyadh Saudi Arabia leo alasiri. Lengo la ziara yake hiyo, ambayo ni ya kwanza tangu alipotangaza hali ya hatari mnamo tarehe 3 mwezi huu, ni kufanya mazungumzo na mfalme Abdaulla Bin Abdel Aziz juu ya mgogoro wa kisiasa nchini Pakistan.

Kumekuwa na ripoti kwamba Saudi Arabia inafanya juhudi kuwakutanisha rais Musharraf na waziri mkuu wa zamani wa Paksitan, Nawaz Sharif, anayeishi uhamishoni mjini Jeddah, nchini Saudi Arabia.

Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa leo na televisheni ya Al Jazeera, Nawaz Sharif amekanusha kuwepo kwa mpango wa kukutana na rais Pervez Musharraf.

Rais Musharraf ameandamana na kiongozi wa huduma za ujasusi nchini Pakistan, luteni jenerali Nadeem Taj. Alitarajiwa kukaa mjini Riyadh kwa muda wa saa chache kabla kwenda Jeddah akielekea kuhiji Mecca.

 • Tarehe 20.11.2007
 • Mwandishi
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CPb2
 • Tarehe 20.11.2007
 • Mwandishi
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CPb2

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com