RIYADH : Mfarakano wa madhehebu kupigwa vita | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH : Mfarakano wa madhehebu kupigwa vita

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran na Mfalme Abdullah was Saudi Arabia wamekubaliana hapo jana kupiga vita majaribio ya kuchochea mfarakano kati ya Wasunni na Washia wakati wa ziara ya kiongozi huyo wa Iran nchini Saudi Arabia.

Ahmedinejad pia ameelezea kuunga mkono kwa nchi yake juhudi za Saudi Arabia kutuliza hali nchini Lebanon na kutatuwa mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali nchini Saudi Arabia SPA viongozi hao wawili wamesisitiza haja ya kuhifadhi umoja wa Iraq na kuhakikisha kuwepo kwa usawa miongoni mwa wananchi wake.

Maelezo rasmi ya mazungumzo yao yametolewa leo hii masaa matatu baada ya Ahmedinejad kukamilisha ziara yake nchini Saudi Arabia ambayo ilikuwa ikitarajiwa kutawaliwa na mfarakano wa madhehebu nchini Iraq,mgogoro wa Lebabon kadhalika mzozo wa nuklea wa Iran na mataifa ya magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com