Ripoti ya jenwefali Pertaeus | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ripoti ya jenwefali Pertaeus

Ripoti inayotatanisha kuhusu hali ya mambo nchini Irak

default

Ripoti ya mkuu wa vikosi vya Marekani nchini Irak,jenerali PETRAEUS iliyokua ikisubiriwa kwa hamu nchini Marekani na kwengineko ulimwenguni,imeshatolewa.Kimsingi ripoti hiyo inapendekeza baadhi ya wanajeshi waanze kuondolewa Irak kabla ya mwaka huu kumalizika.

Kulizuka mkasa hata kabla ya ripoti yenyewe kutolewa.Jenerali Petraeus alipojiandaa kuhutubia mbele ya baraza la Congress,kipaza sauti kikaharibika .Ndo ubaya wa kiufundi.Kwa hivyo wanasiasa,wadadisi na mamilioni ya wasikilizaji na watazamaji wa radio na televisheni wakalazimika kusubiri dakika 15 nzima hadi mkuu wa vikosi vya Marekani nchini Irak alipotamka:

“Nimependekeza idadi ya wanajeshi walioko Irak ipunguzwe.Katika kipindi cha mwezi huu,kikosi maalum cha wanamaji wataihama Irak…Zaidi ya hayo nimependekeza kikosi cha wanajeshi wa kupigana vita wawe wameshaihama Irak hadi ifikapo kati kati ya December,vikosi vyengine vine vya wanajeshi na viwili vya wanamaji watarejea nyumbani katika kipindi cha m,iezi sabaa ya mwanzo ya mwaka 2008.”

Kati kati ya mwezi July mwakani, na kama hali ya usalama itaruhusu,wanajeshi wa Marekani watapunguzwa kutoka laki moja na 60 elfu hivi sasa na kusalia wanajeshi laki moja na 30 elfu.Wanajeshi 30 elfu wa ziada watakua wakiihama hatua baada ya hatua nchi hiyo mnamo miezi hii ya mwisho ya mwaka huu.

Wote wawili , jenerali Petraeus na balozi wa Marekani nchini Irak,Ryan Crocker wametoa picha ya kutatanisha kuhusu hali ya mambo nchini Irak.

Jenerali Petraeus amesema hali imekua bora hasa katika maeneo yanayopakana na Baghdad na katika juimbo la al Anbar.Anahoji mashambulio yamepungua sana katika maeneo hayo.Balozi wa Marekani nchini Irak Crocker anasema kwa upande wake,hakuna maendeleo ya maana yaliyopatikana katika sekta ya kisiasa.Hata hiovyo anaitetea serikali ya mjini Baghdad hasa dhidi ya lawama za wanasiasa wa kimarekani.

“Nnahisi viongozi wa nchi hiyo wanataka kuyashughulikia kikamilifu matatizo yaliyoko,hata kama inachukua miuda mrefu kuliko vile tulivyofikiria.Lakini mazingira na hali yenyewe namna ilivyo hairuhusu mambo kua vyengine.”

Majibu kwa ripoti zote mbili nayo pia yanatofautiana.Wanasiasa wa kutoka chama cha Democratic wanaonyesha wamevunjika moyo.Wanahisi mpango wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi hawendi mbali vya kutosha.Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia siasa ya nje Tom Lantos amefika hadi ya kuwatuhumu moja kwa moja jenerali Petreaus na balozi Crocker,eti wametumwa na serikali ya Bush waje wawatanabahishie wabunge Marekani itashinda vita nchini Irak.Tom Lantos amesema tunanukuu:”Bwana wangu wee,mie siamini msemayo.”Mwisho wa kumnukuu.

Katika wakati ambapo jenerali Petraeus na balozi Crocker walikua wakihutubia bungeni baadhi ya watu walihanikiza kwa makelele na kuzomea.Mara kadhaa kikao hicho kilibidi kusitishwa hadi kilipomalizika saa za usiku.

Hii leo jenerali David Petraeus na balozi Ryan Crocker watalazimika kujibu masuala ya wanachama wa baraza la Senet.Malumbano kati ya wanaopendeelea vita vikome haraka na wale wanaounga mkono vita hivyo hayana dalili ya kumalizika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com