1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya FIFA itachapishwa au la?

12 Desemba 2014

FIFA inakabiliwa na kura wiki ijayo juu ya iwapo ripoti nyeti kuhusiana na madai ya rushwa wakati wa kuomba kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 na 2022, ichapishwe ama la.

https://p.dw.com/p/1E3Pt
Schweiz Fußball FIFA Logo in Zürich
Picha: S. Bozon/AFP/Getty Images

Shirikisho hilo la kandanda litajadili suala hilo katika mkutano wake wa siku mbili wa kamati tendaji utakaofanyika pembezoni mwa pambano la kombe la dunia la vilabu nchini Morocco Desemba 18 na 19.

Ajenda iliyotolewa siku ya Alhamis kwa ajili ya mkutano huo itasikiliza pendekezo lililowasilishwa na Theo Zwanziger, mkuu wa zamani wa shirikisho la kandanda nchini Ujerumani DFB na mkosoaji mkubwa wa uamuzi wa kuipatia Qatar uenyeji wa fainali za mwaka 2022 za kombe la dunia.

Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza limedai kuwa Zwanziger anataka sehemu iliyoondolewa na ripoti kamili ya kamati ya maadili ichapishwe ili kulinda majina ya mashahidi ambao wameshirikiana na kikosi cha uchunguzi uliongozwa na mwanasheria wa Marekani Michael Garcia.

Hadi sasa ni kurasa 42 tu za ripoti hiyo imekwisha chapishwa na jaji wa kamati ya maadili ya FIFA Hans-Joachim Eckert, lakini hatua hiyo imepingwa na Garcia ambaye anadai haina uwakilishi halisi wa ripoti yake.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman