Ripoti: Manchester United yamfuta Van Gaal
23 Mei 2016Matangazo
Rpoti zinasema kuwa Mholanzi huyo amepigwa kalamu na kuwa Jose Mourinho, kocha wa zamani wa Real Madrid na Chelsea anatarajiwa kuchukua nafasi yake.
Shirika la habari la BBC liliripoti kwa mara ya kwanza kuhusu habari hizo siku ya Jumamosi mara tu baada ya Manchester United kushinda Kombe la Shirikisho la Kandanda Uingereza , FA. United iliifunga Crystal Palace mabao mawili kwa moja katika fainali iliyochezwa uwanjani Wembley.
Ripoti za vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza na Uhispania zinasema kuwa wakala wa Jose Mourinho, Jorge Mendes anatarajiwa kuwasili Uingereza wakati wowote ili kukamilisha mkataba huo kabla ya tangazo rasmi kutolewa baadaye wiki hii
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman