Rice kufanya ziara Ethiopia wiki ijayo | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rice kufanya ziara Ethiopia wiki ijayo

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ataitembelea Ethiopia wiki ijayo kwa mikutano juu ya mizozo katika eneo tete la maziwa makuu barani Afrika, Sudan na Somalia .

Rice ambaye sio sana kuzuru Afrika hii itakuwa ni ziara yake ya tatu kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika tokea ashike wadhifa huo wa waziri wa mambo ya nje hapo mwaka 2005.Aliwahi kutembelea Liberia, Senegal na Sudan lakini alifuta ziara yake Afrika mwezi wa Julai uliopita.

Rice atakuwepo katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa hapo Desemba tano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa eneo la nchi za maziwa makuu barani Afrika wa Rwanda, Burundi ,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Uganda na watazungumzia masuala ya amani na usalama kwenye eneo hilo .

 • Tarehe 30.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUws
 • Tarehe 30.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUws

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com