1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

REMBANG: Manusura 200 waokolewa

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeQ

Waokoaji nchini Indonesia wamesema wamefaulu kuwaokoa manura takriban 200 kutoka baharini baada ya feri walimokuwa wakisafiria kuzama kwenye pwani ya kisiwani Java.

Maiti 66 zimepatikana lakini inakadiriwa watu zaidi ya 400 hawajulikani waliko. Hali mbaya ya hewa na kuchafuka kwa bahari kunazuia harakati za uokozi. Feri hiyo ilizama ilipokuwa njiani ikielekea Semarang mkoani Borneo, kisiwani Java, ikitokea bandari ya Kuzmai.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, kwa niaba ya serikali yake, ametuma rambirambi kwa rais wa Indonesia, Susilo Bambang Yudhyono.