1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAWALPINDI:24 wauawa 66 wajeruhiwa katika shambulio la mabomu

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSg

Watu 24 wameuawa na wengine zaidi ya 66 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka kwenye mji wa Rawalpindi nchini Pakistan.

Msemaji wa jeshi la Pakistan amesema kuwa bomu la kwanza lililipuka kwenye basi lililokuwa na wafanyakazi wa wizara ya ulinzi waliyokuwa wakielekea kazini.

Bomu la pili lililihusisha pikipiki kwenye eneo la kibiashara mjini humo, na hakuna taarifa zozote za wahusika wa mashambulio hayo lakini maafisa wa kijeshi wanasema kuwa huenda ni wapiganaji wa kiislam.