1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa amrithi Zuma

19 Desemba 2017

Mkuu wa idhaa za DW zinazolitangazia bara la Afrika, Claus Stäcker amefuatilizia kuchaguliwa Cyril Ramaphosa kuwa mwenyekiti mpya wa chama cha African National Congress. Katika uhariri wake anasema ni uteuzi muwafaka.

https://p.dw.com/p/2pcTd
GMF | Claus Stäcker

Cyyril Ramaphosa ni chaguo muwafaka kabisa kwa Afrika Kusini. Lakini tu kwasababu hakujakuwa na bora kuliko yeye. Bado chama cha ANC kinabakia kuwa chama cha taifa na mpango unaodhihirika kuandaliwa na kambi ya Zuma ili kuendelea kusalia madarakani kupitia aliyekuwa mkewe Nkosazana Dlamini-Zuma, umeshindwa angalao kwa sasa. Ingawa si haki kumteremshia hadhi yake, daktari mzima, aliyewahi kuwa waziri na pia mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma na kumbakishia jina la mke wa zamani wa Jacob Zuma. Lakini pekee dhana ya kuibuka utawala wa familia, na makundi yanayouunga mkono na hasa mkondo wa kisiasa wanaoufuata, vingekuwa kizingiti kwa mwanzo mpya.

Wakulima na jamii za wachacheb wameshusha pumzi

Kuchaguliwa Ramaphosa ni afadhali kuliko chaguo jengine. Masoko ya hisa yanashangiria, sarafu ya Afrika Kusini Rand imepanda thamani  kwa nukta nne dakika chache baadae. Wakulima wanashusha pumzi, jamii za wachache, tangu wenye asili ya kizungu mpaka  ya kihindi wamepowa. Ramaphosa anasifiwa kuwa mtu mwenye uwezo wa kuleta wizani wa kisiasa, mwenye ujuzi wa kiuchumi na pia mwenye kuheshimu mwongozo wa serikali na hasa nje ya chama cha ANC. Njia aliyoifuata imemchukua miaka 20 hadi kufikia kileleni mwa African National Congress-ANC. Tayari katika uhai wake Nelson Mandela alifikiria kumgeuza Ramaphosa awe mrithi wake, lakini alishindwa kutokana na upinzani wa ndani chamani.

Katika wakati ambapo waliberali na wanauchumi wanamsifu kuwa msimamizi mwema na mwenye kutambua ukweli wa mambo, wafuasi wa siasa kali na watu wasiojimudu wanamwangalia Ramaphosa kuwa mtu asiyejali chochote, mtu aliyepanda daraja kutoka mwanaharakati wa haki za wafanyakazi na kugeuka tajiri mkubwa anaetajikana kuwa miongoni mwa matajiri kumi wakubwa kabisa mwenye asili ya kiafrika nchini humo. Anakosolewa zaidi tangu yalipotokea mauwaji ya Marikana mwaka 2012, alipowataja wachimba migodi waliokuwa wakigoma kuwa "wahalifu". Na ingawa Ramaphosa aliomba radhi baadae, hata hivyo dowa tangu wakati huo halijatakasika miongoni mwa jamii ya wafanyakazi.

Kinyang'anyiro cha kupimana nguvu cha hofiwa ndani ya ANC

Hadhi yake imechujuka pia alipokuwa makamo wa rais wa Jacob Zuma, ambapo miaka mitatu haikumsaidia kuzuwia visa vya rushwa na ufisadi. Wengi walitarajia angepiga vita rushwa na kupigania uwazi, badala yake alikuwa sawa na simba asiyekuwa na meno. Sawa na wanachama wengine kadhaa wa ANC , na yeye pia alibakia kufuata mwongozo wa chama.

Katika njia ya kuelekea kileleni Ramaphosa hajapoteza pekee sifa yake, hata kile anachokipigania kimefutwa. Ramaphosa ataingia katika kampeni za uchaguzi mwaka 2019 akiwa katika hali dhaifu. Nchi hiyo inadaiwa kupita kiasi na hajui fedha zitatokea wapi. Na kutokana na jinsi Zuma alivyoshangiriwa katika hotuba yake ya kuaga, hali hiyo inaashiria mashindano ya kupimana nguvu ndani ya ANC.

 

Mwandishi:Claus Stäcker/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Iddi Ssessanga