RAMALLAH: Serikali ya dharura ya Wapalestina imeapishwa Ukingo wa Magharibi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Serikali ya dharura ya Wapalestina imeapishwa Ukingo wa Magharibi

Serikali mpya ya dharura ya Wapalestina imeapishwa hii leo mjini Ramallah,kwenye Ukingo wa Magharibi.Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah,amelitangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kuivunja serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Hamas na Fatah.Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya wanamgambo wa Hamas kuudhibiti Ukanda wa Gaza,kufuatia mapigano makali.kwa upande mwingine,Israel imekaribisha uteuzi wa baraza hilo jipya la mawaziri.Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amesema,serikali isiyokuwa na mawaziri kutoka chama cha Hamas, inaashiria nafasi mpya ya kupata amani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com