1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Abbas apendekeza kuundwe baraza la mawaziri la wasomi

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1i

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, amependekeza kuundwe baraza la mawaziri la mpito litakalojumuisha wasomi, baada ya juhudi za kuunda serikali ya umoja wa taifa kugonga mwamba.

Lakini chama tawala cha Hamas kinasisitiza kwamba serikali ya muungano itakayojumuisha makundi mbalimbali ndilo chaguo zuri.