RAMALLAH: Abbas ameihimiza Israel irejee kwenye majadiliano
16 Novemba 2006Matangazo
Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina ametoa mwito kwa Israel kurejea kwenye meza ya majadiliano. Amesema Wapalestina wapo tayari kufanya majadiliano ya dhati kuumaliza mgogoro wa miongo kadhaa.Abbas ameihimiza Israel kutoiacha nafasi ya kupata amani.