1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Zambia amlaumu Gordon Brown

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXi1

BERLIN.Rais Levy Mwanawasa wa Zambia ameushutumu uamuzi wa Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown kwa kususia mkutano wa kilele kati ya Afrika na Ulaya mjini Lisbon Ureno, akipinga kuwepo kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Katika mazungumzo yake hapo jana mjini Berlin na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais Mwanawasa alilaumu aumuzi huo wa Waziri Mkuu wa Uingereza na kusema hiyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwake kuelezea matakwa yake kwa Zimbabwe.

Kwa upande wake Kansela Merkel alisema nchi za Umoja wa Ulaya zinaheshimu uamuzi huo wa Uingereza, lakini wao watahudhuria kwani ni nafasi adhimu kujadili masuala kadhaa muhimu.

Kansela Merkel hata hivyo amesema kuwa suala la Zimbabwe litajadiliwa katika mkutano huo unatarajiwa kuanza Jumamosi katika mji mkuu wa Ureno Lisbon.

Mkutano huo unafanyika baada ya kushindwa kufanyika katika kipindi cha miaka saba iliyopita baada ya ule uliyofanyika Ccairo Misri mwaka 2000.