Rais wa zamani wa Argentina ashtakiwa kuhusiana na biashara haramu ya silaha | Habari za Ulimwengu | DW | 09.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais wa zamani wa Argentina ashtakiwa kuhusiana na biashara haramu ya silaha

Rais wa zamani wa Argentina Carlos Menem ameshtakiwa rasmi kwa mara ya pili kufuatia madai ya kuhusika na biashara haramu ya silaha kwa Croatia na Ecuador katika miaka ya tisini.

Aliwahi kukabiliwa na mashataka kama hayo mwaka 2001 lakini yalifutiliwa mbali baada ya kuwekwa chini ya kifungo cha ndani ya nyumba kwa miezi mitano kuhusiana na kesi hiyo.

Menem hata hivyo amekanusha mashtaka dhidi yake.Menem mwenye umri wa miaka 77 alikuwa rais wa Argentina kutoka mwaka 1989 hadi mwaka 1999 na amesema anatumai kugombea tena wadhifa huo katika uchaguzi mkuu wa mwezi October licha ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa gavana katika jimbo lake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com