Rais wa Ujerumani Wulff atoa ujumbe wa Krisimasi
24 Desemba 2011Matangazo
Rais Wulff ameyasema hayo kuhusiana na mfululizo wa mauaji yaliyofanywa na kundi la mafashisti mamboleo katika jimbo la Thuringia, mashariki mwa Ujerumani.
Rais wa Ujerumani amesema, matukio hayo yaliyokuwa na hulka za uhalifu wa kibaguzi yaliwashtua watu wote.
Katika ujumbe wake Rais Wulff pia amewataka watu wawe macho na tayari kutetea demokrasia, maisha na uhuru wa wananchi wote wa Ujerumani.
Rais wa Ujerumani pia alizungumzia juu ya mgogoro wa madeni barani Ulaya na amewataka watu wawe na moyo.
Amesema, ana uhakika kwamba itawezekana kupatikana njia ya kuufumbua. Pia amehakikisha kwamba Ujerumani itaendelea kuwa na msimamo wa mshikamano barani Ulaya.