1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ufaransa ziarani Afrika

P.Martin27 Julai 2007

Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy amependekeza ushirikiano kati ya Ulaya na Afrika.

https://p.dw.com/p/CHAR
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akikaribishwa na Rais Muammar Gadaffi wa Libya mjini Tripoli
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akikaribishwa na Rais Muammar Gadaffi wa Libya mjini TripoliPicha: AP

Alipozungumza mbele ya wanafunzi katika mji mkuu wa Dakar, wakati wa ziara yake nchini Senegal,Sarkozy aliongezea kuwa ushirikiano huenda ukasaidia kupunguza athari za utandawazi na ukachangamsha maendeleo.Akasema,ukoloni ulioanzishwa barani Afrika ni kosa kubwa,lakini Waafrika pia,kwa sehemu fulani,wamechangia hali ya kukosekana kuwepo maendeleo zaidi.Sarkozy,alikutana pia na Rais Abdoulaye Wade wa Senegal na wanasiasa wa upande wa upinzani.

Ziara ya Sarkozy,ilianzia Libya ambako alitia saini mkataba unaohusika na mtambo wa nishati ya nyuklia.Mkataba huo umekosolewa na serikali ya Ujerumani na mashirika yanayohusika na mazingira.Sarkozy lakini,ameutetea mkataba wa kupeleka Libya teknolojia ya nyuklia.Amesema, nchi za Kiarabu zisizuiliwe kuwa na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.

Baadae leo hii,Rais Sarkozy ataelekea Gabon,nchi yenye utajiri wa mafuta.